Wito wa kampeni ya umoja wetu
- Miaka 125 tangu kunfanyika mkutano wa Berlin
- kuhusu Bara la Afrika: kumbuka - tathmini - fidia
-
Miaka 125 iliyopita wakati wa kipindi cha baridi 1884/85 kansela wa Ujerumani, Bismark aliwakaribisha wawakilishi toka dola kubwa duniani katika mkutano wa Afrika, uliojulikana pia kama “Congo conference”. Kwa kile walichokiita kama sababu za kimaendeleo na kiutu chini ya itikadi za za ulaya za kibaguzi, jumla ya nchi 12 za ulaya , dola la Osman na Marekani zilikubaliana kuligawa bara la Afrika katika makoloni na kunyonya mali za Afrika. Katika ukumbi wa mkutano wa kansela bonde la Kongo lilikabidhiwa kwa mfalme wa Ubeligiji Leopold wa pili. Utawala wake wa kikatili ulisababisha vifo vya zaidi ya watu milioni kumi. Katika mkutano huo Ujerumani ilikuwa miongoni mwa wakoloni. Hukuma za kupiga viboko, uporaji wa watu na mali, kazi ngumu, mateso, ubakaji, kambi za maangamizi na mauaji yalisa babisha vifo vya watu laki nne katika kipindi cha miaka thelathini ya ukoloni wa wajerumani katika nchi ambazo hivi sasa ni Namibia, Togo, Cameroun, Tanzania, Burundi na Ruanda katika mapambano dhidi ya ukoloni. Hata hivyo historia ya ukoloni wa Ujerumani na nchi za ulaya kamwe hazizungumzi madhila ya ukoloni. Wakati wakitukuza ukoloni, hufumbia macho madhila kama kwamba hayakufanyika na hayakuwa muhimu katika ukoloni wa kijerumani.
Ukoloni na madhila yake wala hayatathminiwi katika taasisi za elimu, vyama vya siasa au katika vyombo vya habari au kufanyiwa utafiti. Hakuna kumbu kumbu yeyote iliyowekwa hadharani inayohusu wahanga wa ukoloni wasiokuwa na idadi. Tarehe 23. August, siku ya kimataifa ya kukumbuka biashara ya utumwa na upigaji marufuku biashara hiyo haipewi uzito wowote nchini Ujerumani. Kinyume chake wahalifu wa kikoloni wa kijerumani wanaenziwa na kukumbukwa mitaani, sehemu tofauti na barabarani. Bila kukosoa na kuona vibaya makumbusho ya ujerumani yanaonesha sanaa na mali zilizoporwa kutoka nchi zilizokuwa makoloni yao. Hadi leo bado kuna mabaki ya waafrika katika ghala na makumbusho nchini ujerumani kwa matumizi ya utafiti wa kibaguzi. Miaka 125 tangu mkutano wa Afrika uliofanyika Berlin bado hakuna tathmini ya kina iliyofanyika juu ya ukoloni.
Madhila ya ukoloni bado hayajakomeshwa sio tu Ujerumani bali pia katika nchi zilizokuwa makoloni. Mizozo ya kijamii na kisiasa iliyopo katika nchi zilizokuwa makoloni inatokana na kupandikiza kwa fikra za kikoloni na mifumo ya kijamii kulikofanywa na wakoloni weupe. Hadi leo biashara ya silaha kutoka ulaya inapalilia mizozo iliyopo. Kwa kiasi kikubwa miundo ya kiuchumi na kisiasa ya kimataifa zimetokana na nyakati za kikoloni. Sera za nchi za ulaya juu ya maendeleo zinazidisha tofauti badala ya kuondoa. Mikataba ya kiuchumi ikiwemo ya mashirikiano ya kiuchumi, EPA inaathiri soko la bidhaa za Afrika katika nchi za ulaya badala ya kudumisha. Kwa upande mwingine nchi za ulaya zinajinufaisha zaidi na mali asiri za bara la Afrika. Wakati huo huo mamia ya waafrika wanapoteza maisha yao katika mipaka ya ulaya huku wakimbizi wakiwekwa maabusu kusubiri kurejeshwa makwao. Ubaguzi unatokana kwa kutumia mabavu ya kimwili, kiakili pia kwa ubaguzi wa kisheria dhidi ya watu weusi na rangi tofauti. Chanzo cha Ubaguzi kinatokana na wakati wa ukoloni. Ukoloni bado hupo na unaongoza jamii yetu ya sasa.
-
Katika kuadhimisha miaka 125 tangu kufanyika mkutano wa Afrika mjini Berlin tunatoa wito wa kuwa na msimamo dhabiti dhidi ya ukoloni wa ujerumani uliopita!
-
Wito wetu:
Kumbuka
Kuadhimishwa siku ya kimataifa juu ya biashara ya utumwa na kupingwa marufuku biashara hiyo tarehe 23 August
Kutayarishwa mabango maalum yatakayowekwa hadharani
Kubadilisha majina ya mitaa, ambayo yanaenzi wakoloni au kuashiria ubaguzi, badala yake yawaenzi mashujaa waliopambana dhidi ya ukoloni
Tathmini
Shughuli za kukosoa ukoloni na ubaguzi wa rangi mashuleni, vyuoni, hadharani na makanisani
Ufadhili wa harakati dhidi ya ukoloni na utamaduni wa ubaguzi wa rangi pamoja na miradi ya kisiasa
Ushirikiano katika miradi ya utafiti na taasisi za elimu na nchi zilikuwa makoloni ya kijerumani
Shirika la kijerumani la kuweka kumbukumbu na kutathimini ukoloni uliopita
Hatua kamili zitakazotokomeza mfumo unaowabagua watu weusi na rangi nyengine katika taasisi za kielimu na kisiasa pia katika sehemu nyengine za kijamii
Kuondosha sheria za kibaguzi na za uajiri zitakazofuatana na mabadiliko ya sheria zinazokiuka haki za binadamu katika sera za uhamiaji
-
Fidia
Kutambua kuwa ukoloni wa kijerumani na wa nchi za ulaya kuwa ni uvunjaji wa haki za binadamu
Kubeba majukumu ya kihistoria kutokana na uvunjaji wa haki za binadamu
Kufidia kihali na mali madhara ya ukoloni wa kijerumani na nchi nyengine za ulaya (misaada ya fedha inayotolewa siyo fidia!)
Tarehe 16 Septemba 2009 Berlin
Ninasaini wito kama mtu binafsi
Tunaunga mkono kampeni kama shirika:
Diese E-Mail-Adresse ist gegen Spambots geschützt! JavaScript muss aktiviert werden, damit sie angezeigt werden kann.
|