Karibu katika tuvuti ya umoja wetu
Kwa mwaliko wa Serikali ya Ujerumani wawakilishi kutoka dola kubwa duniani walikutana mjini Berlin tarehe 15 Novemba 1884. Azma kubwa za mkutano huo wa Berlin wa uliojulikana pia kama Congo-conference ilikuwa kukubaliana kugawana na kulitawala bara la Afrika. Mamilioni ya waafrika walipoteza utu, mali na maisha yao kutokana na ukoloni huo wa nchi za ulaya.
Umoja wetu unatoa wito kwa jamii kuwa na msimamo dhabiti dhidi ya ukoloni uliopita. Tunatoa wito wa kupinga ukoloni pamoja na mizizi ya ubaguzi wa rangi. Tunatarajia Ujerumani na nchi za ulaya zitabeba majukumu ya kihistoria kutokana na madhila ya ukoloni pamoja na kuchukua hatua muwafaka za kutoa fidia.
Kampeni ya Umoja wetu ni shirikishi: Una furasa kutumia tuvuti yetu kushiriki kupanga, na kutoa mawazo yako. Unaweza kufanya yafuatayo:
- Kusaini wito wetu wa kampeni
- Kurekebisha mpango wetu wa siku ya maadhimisho (
Diese E-Mail-Adresse ist gegen Spambots geschützt! JavaScript muss aktiviert werden, damit sie angezeigt werden kann.
) - Kuchangia, hati, maoni juu ya sababu za kihistoria ( Diese E-Mail-Adresse ist gegen Spambots geschützt! JavaScript muss aktiviert werden, damit sie angezeigt werden kann. )
- Kupendekeza aina ya fidia
- Kuchangia kifedha kampeni yetu ya kujitolea
Tunatoa shukrani zetu kwa mashirtikiano yenu!
|

